Kikizungumza na Ijumaa Wikienda kutoka London, Uingereza, wikiendi iliyopita, chanzo hicho makini kilisema mwanaume ambaye hivi karibuni Shilole alijinadi kuwa ni bw ana’ke siyo kwani huko London baadhi ya watu wanamfahamu kama mwanaume tata kijinsia.“Yule jamaa anapenda sana kukaa na wanawake, sijawahi kumuona na wanaume wenzake, kazi kukata tu mauno na wanawake. Nilishangaa sana Shilole kusema eti ni mc humba’ke wakati hapa London (Uingereza) ni maarufu sana kwa kushiriki pati za wanawake. “Maskini Shilole, pale imekula kwake, hakuna chochote,” kilisema chanzo hicho. Baada ya kunyetishiwa habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Shilole ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Jamani imeniuma sana kwani nilikuwa sijui, nimeligundua hilo baada ya kuambiwa na watu, nilipigiwa simu kutoka Uingereza kwamba yule mwanaume siyo hivyo sina mpango naye tena kwa kweli,” alisema Shilole anayetamba na kideo cha Nakomaa na Jiji.
GPL
No comments:
Post a Comment