MTUME na Nabii wa Kanisa la Efatha, Joseph Elias Mwingira
anayekabiliwa na kesi ya kuzaa na mke wa mtu, hatimaye amefunguka mengi
kuhusu madai hayo lakini amekataa kabisa kupima Ukimwi, Risasi
Mchanganyiko lina kila kitu.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi -
Kisutu, Dar, umebaini kuwa Mwingira aliye na kesi mahakamani hapo yenye
namba 306 ya 2013, iliyofunguliwa na mlalamikaji Dk. Morris William,
amejibu tuhuma zinazomkabili kwa njia ya maandishi.
Majibu hayo yameandaliwa na Kampuni ya Uwakili ya Legal Link, ambapo
nakala yake imefikishwa kwa wakili wa mlalamikaji Dk. William, Januari
22, mwaka huu.
Pamoja na mambo mengine, madai yaliyopo katika jalada la kesi hiyo,
mlalamikaji Dk. William, ameomba mahakama ikubali Nabii Mwingira apimwe
Ukimwi na kipimo cha utambuzi wa vinasaba ‘DNA’.
Nabii huyo amepinga vikali ombi hilo, akieleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo (la madai ya kifedha).
MADAI YA MAPENZI
Katika majibu hayo (nakala
tunayo), Mwingira amekanusha kufanya mapenzi na mlalamikiwa namba mbili,
Dk. Phillis Nyambi ambaye ni mke wa mlalamikaji.
“Mlalamikiwa namba
moja amefafanua kuwa hakuingia katika uhusiano wa kimapenzi na
mlalamikiwa wa pili,” imeeleza kampuni inayomtetea Mwingira.
AKANA KUBAKA
Nabii huyo pia amekanusha madai ya
kumbaka mlalamikiwa wa pili kama alivyosema mlalamikaji katika hati yake
ya malalamiko iliyopo mahakamani hapo.
Nabii Mwingira pia amekana
madai ya kuzaa na mlalamikiwa namba mbili na kuwepo kwa matatizo ya
kitabibu kwa mama huyo ambaye sasa ana mtoto mwenye umri wa miaka
mitano, akasema mlalamikaji anatakiwa kuthibitisha.
Kuhusu madai ya Dk. Phillis kushiriki kimapenzi na Mwingira hivyo
kusaliti ndoa halali na kumharibia furaha ya maisha mlalamikaji, nabii
huyo amesema hajawahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na mwanamke
huyo.
Kuhusu madai ya Mwingira kutembea na mke wa mlalamikaji na habari
hizo kuandikwa magazetini na kwenye mitandao ya kijamii hivyo
kumdhalilisha na kumshushia hadhi, amedai kuwa yeye hahusiki na hilo na
atahitaji kuthibitisha.
Madai mengine ya mlalamikaji kwamba vitendo vya walalamikiwa namba
moja na namba mbili vya kujihusisha kimapenzi vimemuathiri Dk. Morris
kisaikolojia na kiuchumi na kumfanya apoteze biashara zake za kimataifa
kwa kukosa wadhamini katika NGO yake, Mwingira amesema kama yametokea
hakuyasababisha yeye.
Ameiomba mahakama kuitupilia mbali kesi hiyo na kumuamuru mlalamikaji
kulipa gharama za kesi hiyo, hivyo ameweka pingamizi la awali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment