MWANAMKE AJIFUNGUA FARASI KANISANI, CHEKI HAPA


Waumini wa kanisa la ‘World liberation Ministry’ linalopatikana katika mji wa Sepele nchini Benin walikumbwa na mshangao baada ya mwanamke mmoja kujifungua farasi wakati wa misa ya maombi iliyofanyika katika kanisa hilo.

Hata hivyo wakati waandishi wa habari walipofika katika kanisa hilo, tayari farasi huyo alikuwa ameshakufa. Inasemekana kuwa mwanamke huyo ambaye jina lake bado halijajulikana, alianza kupiga kelele wakati wa maombi na kisha kuanza kutoa damu katika sehemu zake za siri kabla ya kujifungua farasi huyo.

Msimamizi mkuu wa kanisa hilo, muinjilisti Silva Wealth alisema kuwa bado anashangazwa na kilichomtokea mwanamke huyo. Silva alisema kuwa wakati wa maombi alipata uono kuwa kuna mwanamke mwenye tatizo na kwamba kulikuwa kunakitu kinazuia...

Silva aliendelea kusema kuwa maombi yalipopamba kasi, mwanamke huyo alianza kupiga kelele kisha damu zikaanza kumtoka halafu kikamtoka hicho kitu.

“Siwezi kuelezea kitu hicho. Katika maombi yetu tumewahi kushuhudia watu wakitapika vitu mbalimbali, lakini sio kitu kama hiki.” Alisema muinjilisti Silva.

Mara baada ya taarifa hizo kuzagaa mitaani, watu mbalimbali walianza kukimbilia katika kanisa hilo ili kuweza kushuhudia kwa macho yao.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger