MWANAMKE AMUUA MWANAE WA MWEZI MMOJA KWA VIDONGE VYA USINGIZI.



MWANAMKE mmoja mkazi wa Nakuru nchini kenya alitiwa nguvuni mnamo siku ya jumanne kwa tuhuma ya kumpa Vidonge vingi mtoto mchanga Chanzo cha habari kikieleza kwamba kisa cha kufanya hivyo ni kurahisha safari zake za kwenda kujirusha na wenzie.

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina 'Grace Wambui', Alimueleza Hakimu 'Enyara Emukule' wa mahakama kuu kwamba alimshindilia vidonge hivyo vya usingizi mtoto huyo mwenye umri wa mwezi mmoja ili alale usingizi mzito asimkere kwa kulialia.

Ilmradi apate nafasi ya kutoka na wanawake wenzie ambao walikuwa wakijihusisha na biashara ya kuuza mwili (Uchangudoa) lengo likiwa nikutafuta pesa za kujikimu kimaisha kwa kuwahudumia watoto wake wengine wakubwa zake na huyo aliyemezeshwa vidonge.

Lakini kwa bahati mbaya baada ya kukamilisha zoezi hilo alielekea moja kwa moja mihangaikoni na kujipatia vijisenti vya kujikimu kama kawaida, Sasa basi..! Siku ya tukio Grace Wambui alipotia maguu nyumbani kwake alikuta majirani wamejazana top! Kumbe maskini wa mungu yule kiumbe ameaga dunia kupitia vidonge vya usingizi alivyomshindilia.

Kumbe majirani walishapiga simu polisi..!,Huku na kule akashangaa polisi wametia timu na kumtia mbaroni mpaka sasa anasubiria kusomewa mashtaka Wiki Ijayo.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger