Neymar amemtetea baba yake
katika sakata la dili la 86.2 million euro lilomleta mshambuliaji
Barcelona katika kipindi cha kiangazi kilichopita, na inaonekana dili
hilo liliingizia familia yake kiasi cha 51.2 million euros kama gharama
ya kufanikisha uhamisho wa mchezaji huyo. (HM)
Mahakama moja nchini Spain kwa
sasa inafanya uchunguzi kuangalia kama kuna mchezo wowte mchafu
ulifanyika katika uhamisho huo, wakati tayari Sandro Rosell
ameshajiuzulu kama raisi wa Barca mwezi uliopita kutokana na sakata
hili.
A
Uhamisho wa Neymar unachunguzwa nchini Brazil,
huku klabu ya zamani ya Neymar Santos na taasisi ya uwezekezaji ya DIS
Esporte wakisema wanahitaji kulipwa zaidi kutokana na dili hilo.
Wote
Neymar Snr na Barca wanasisitiza hakuna kitu chochote kilichoenda
kinyume kisheria wakati wa uhamisho huo, huku Barca wakichukua hatua
nyingine kuelezea malipo ya 40
million euros waliyolipa kampuni ya N&N -- inayomilikiwa na wazazi
wa Neymar --- 2.7 million euros alilipwa Neymar Snr kama kamisheni, pia
kuna malipo mengine ya makubaliano ya kibiashara na taasisi inayodili na
mchezaji, yote ambayo yanafikia jumla ya 8.5 million euros.
Leo hii Neymar alitumia akaunti yake ya mtandao wa Instagram kuandika ujumbe ufuatao kuhusu uhamisho wake.
Leo hii Neymar alitumia akaunti yake ya mtandao wa Instagram kuandika ujumbe ufuatao kuhusu uhamisho wake.
"Niliamua kufunga mdomo wangu mpaka hivi sasa, lakini siwezi kuendelea tena, kusikiliza ujinga unaozungumziwa kuhusu uhamisho wangu. Nilimpigia simu baba yangu nikamwambia nataka nizungumze kuhusu suala hili, lakini alinikataza na kuaniambia nikae kimya na kuweka umakini katika kujiangalia vizuri ili niweze kupona haraka, akisema hili suala lilikuwa likimhusu yeye.
Lakini atanielewa kwanini nafanya hivi. Niliwaomba watu ninaofanya nao kazi wanisaidie kuandika. Nisamehe baba kwa kutokukusikiliza kwa mara ya kwanza, lakini nitaongea.
"Napenda kukushukuru kwa namna ulivyoweza kushughulikia maisha yangu ya soka, biashara ulizozitengeneza kuzunguka kazi yangu na namna ulivyoweza kuitunza familia yetu. Kama niliichezea klabu iliyopo moyoni mwangu Santos na leo naitumikia klabu ya ndoto zangu Barcelona - yote hii shukrani zije kwako
"Nafahamu watu wengi wanaongea ujinga kutuhusu, hata kuwa na mashaka na maadili yetu.....vilevile nimegundua kiasi cha marafiki wanafki tulionao....Baba, wakati Thiago Silva aliposema atakufa kwa ajili yangu uwanjani, na mimi pia nilikuwa tayari kumfanyai hivyo yeye. Lakini kwako wewe baba, sitokuwa tayari kufa mimi tu bali nitayatoa maisha hata ya mwanangu kwa ajili yako!"Kwa hili nakuomba.....rudi Hispania, nakukumbuka. Siku chache zijazo nitarudi kucheza na nakuhitaji uwe hapa. Muda utaonyesha hujafanya kosa lolote. Kwamba ulikuwa tu bi baba bora kwangu. Nakupenda."
No comments:
Post a Comment