TBS: OPERESHENI MITUMBA NI YA KISHERIA


Operesheni mitumbaSHIRIKA la Viwango nchini (TBS) limesema linatekeleza operesheni ya kuondoa nguo za ndani za mitumba kwa kufuata sheria, si kwa ajili ya kuwanufaisha wafanyabiashara wa maduka nchini.
Akizungumza na Tanzania Daima  jana, Ofisa Habari wa shirika hilo, Roida Andusamile, alisema zoezi hilo linatekelezwa kwa mujibu wa sheria na limehusisha wadau wa idara zote.
Alisema ni muhimu Watanzania wakaelewa kuwa kuna athari kubwa inayoweza kuwapata kutokana na kuvaa nguo hizo ambazo zinatoka nje ya nchi.
“Hili zoezi limefanyika kwa mujibu wa sheria na wala hakuna mtu au mfanyabiashara anayebebwa …sisi nia yetu ni kuhakikisha nguo hizo za ndani haziingizwi sokoni kutokana na athari yake,” alisema.
Alisema ni vema Watanzania wakajiepusha na maneno yasiyo na ukweli kuwa zoezi hilo linafanyika kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara wa nguo mpya hasa wale wa madukani.
Ofisa habari huyo alisema kuwa kama suala lingekuwa kutekeleza hayo basi shirika hilo lingepiga marufuku uingizwaji wa nguo zote za mitumba nchini.
TBS imepiga marufuku biashara ya uuzwaji wa nguo za ndani za mitumba zinazoingizwa kwenye soko la hapa nchini na inaendesha operesheni ya kutokomeza nguo hizo katika mikoa mbalimbali nchini.
-Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger