UFAHAMU UNDANI WA VIFO VYA ASKARI POLISI WATANO KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA AJALI YA BASI NA GARI DOGO MKOANI DODOMA. SOMA ZAIDI HAPA
ASKARI Alisema walikuwa na sherehe ya kuwaaga askari wenzao 10 ambao wamestaafu sambamba na kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 ambazo zilifanyika hadi saa sita usiku ndipo askari hao wa Wilaya ya Kongwa waliamua kusafiri wakati huo na kurudi kituoni kwao.
Kutokea kwa ajali hiyo kumethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, David Misime aliyesema ilitokea juzi saa 6:15 usiku katika eneo la Mtumba nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma wakati askari hao wakitokea Dodoma kwenye sherehe za Polisi za kuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014.
Gari la Polisi lilikuwa likiendeshwa na Deogratius Mahinyila huku basi likiendeshwa na Juma Mohamed aliyekimbia baada ya ajali hiyo na polisi wanaendelea kumtafuta.
Aliwataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni D.9084 Adolf Silla (51),F.6459 Evarist Bukombe (34),H.3783 Deogratius Mahinyila (29),WP.10337 Jackline Tesha (22) na WP.10382 Jema Luvinga (20).
Kamanda Misime alisema vifo hivyo ni pigo kubwa kwa Jeshi la Polisi mkoani hapa na kueleza sababu za vifo hicho ni mwendo kasi.
Alisema ajali hiyo imeacha pengo kubwa kwa Jeshi la Polisi kwani wapiganaji hao ambao baadhi wamekufa wakiwa vijana, walikuwa bado wanahitajika na taifa.
Alisema walikuwa na sherehe ya kuwaaga askari wenzao 10 ambao wamestaafu sambamba na kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 ambazo zilifanyika hadi saa sita usiku ndipo askari hao wa Wilaya ya Kongwa waliamua kusafiri wakati huo na kurudi kituoni kwao.
Pia alisema kilichothibitisha kuwa basi lilikuwa katika mwendo kasi ni namna gari dogo walilokuwa wamepanda askari hao jinsi lilivyoburuzwa na basi kwa umbali wa mita 56 na basi kwenda kusimama umbali wa mita 97.
Hata hivyo alisema miili ya askari hao imehifadhiwa katika chumba cha maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kusubiri taratibu za kusafirisha kwa maziko.HABARILEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment