Ubalozi
wa Marekani Kampala wasema kuna ishara kwamba jumba la makumbusho la
kitaifa ni mojawapo ya majengo yanayolengwa na magaidi
Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umeonya juu ya uwezekano wa kutokea shambulizi la kigaidi katika mji mkuu wa Kampala.
Ubalozi wa Marekani nchini Uganda umeonya juu ya uwezekano wa kutokea shambulizi la kigaidi katika mji mkuu wa Kampala.
Taarifa hiyo inaongeza kuwa kuna ishara kwamba jumba la makumbusho la kitaifa ni mojawapo ya majengo yanayolengwa. Lakini serikali ya Uganda haijatoa tamko la haraka juu ya onyo hilo.
Ujumbe huo haujawaonya Wamarekani kuondoka Kampala lakini umewatahadharisha kuepuka jumba la makumbusho na maeneo mengine yenye watu wengi.
Kundi la al-Shabab kutoka Somalia lilifanya shambulizi la kigaidi huko Kampala Julai 2010 na kuuwa watu 70.
Chanzo, voaswahili.com
No comments:
Post a Comment