AUNT AKUMBUKA KIPIGO CHA KUAMBIANA

Stori: Mwandishi Wetu
WAKATI staa wa muvi za Kibongo, Adam Kuambiana akizikwa jana jijini Dar es Salaam, msanii mwenzake Aunt Ezekiel amekumbuka kipigo alichoangushiwa na Kuambiana yeye na Wema, wiki chache zilizopita.

Mrembo Aunt Ezekiel.
Akiteta na kona hii, jana jijini Dar, Aunt alisema: “Nakumbuka hiyo siku, tulikuwa location, Mikocheni mimi, Wema, Martin Kadinda na wasanii wengine tukirekodi filamu ya Wema. Kuna kitu tulikosea, Kuambiana akatupiga mimi na Wema.
“Alikuwa makini sana na kazi yake, hakupenda mzaha unapofika muda wa kazi. Nikikumbuka ile siku huwa namkumbuka sana Kuambiana kwa kweli. Mungu ampumzishe kwa amani.”

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger