Kundi la wapiganaji wa kiislamu
la Al Shabaab limeshambulia bunge la Somalia na kusababisha vifo vya
watu kadhaa mjini Mogadishu.
Milipuko na milio ya risasi imesikika huku bunge likishambuliwa, wabunge wakiwa ndani kwa mkutano.Wabunge pamoja na wafanyakazi wengine waliweza kuokolewa punde baada ya gari kulipuka.
Mashambulizi hayo bado yanaendelea huku wapiganaji hao walifyatua risasi wakiwa ndani ya msikiti mmoja karibu majengo ya bunge.
'Bunge la Somalia'
Serikali ya Somalia imekuwa ikiendesha vita dhidi ya kundi la kiisilamu la al-Shabab ambalo lilitimuliwa kutoka mjini Mogadishu mwaka 2011.
Bunge hilo, ambalo huendesha vikao vyake mjini Mogadishu limewahi kushambuliwa ikiwemo mwaka 2009 na 2010.
Mwezi jana Mbunge mmoja aliuawa kwa kulipuliwa huku mwingine akipigwa risasi na kuuawa katika mashambulizi mawili tofauti.
Wanajeshi 22,000 walio chini ya muungano wa Afrika wanasaidia vikosi vya Somalia kupambana na Al Shabaab.
Ingawa kundi hilo limepoteza udhibiti mkubwa wa miji kadhaa nchini Somalia, bado linadhibiti maeneo mengi ya vijijini.
Chanzo bbcswahili
No comments:
Post a Comment