CHOPA APONGEZWA KUMSITIRI KUAMBIANA, HII NI BAADA YA WASANII KUGOMA

STAA wa filamu wa Bongo Movies, Juma Chikoka ‘Chopa Mchopanga’ amepongezwa na wasanii wenzake kufuatia kitendo cha kumstiri kwa mavazi marehemu Adam Kuambiana aliyefariki dunia Mei 17, mwaka huu na kuzikwa Jumanne iliyopita jijini Dar es Salaam.
Staa wa filamu wa Bongo Movies, Juma Chikoka ‘Chopa Mchopanga’ akiwa na wasanii wenzie katika mazishi ya Kuambiana.
Imeelezwa kuwa, siku ya Jumatatu ambayo mwili wa marehemu ulitakiwa kuogeshwa na kuvishwa nguo, mastaa walisita kufanya kazi hiyo kutokana kuogopa maiti ndipo Chopa kwa mapenzi ya dhati alimbadilisha nguo.
“Nampongeza sana Chopa kwani ndiye aliyemvalisha nguo marehemu na kumalizia pete ya ndoa kwani kila msanii aliogopa kusogelea maiti ya Kuambiana,” alisema msanii mmoja ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger