BAADA
ya kupewa taarifa za msiba wa Adam Kuambiana, staa wa filamu za
Kibongo, Coletha Rymond ‘Koleta’ alijikuta akizimia na kulazwa katika
Hospitali ya Kairuki jijini Dar.
Sosi
ambaye ni mtu wa karibu na staa huyo, alipenyeza habari kuwa Koleta
alishindwa kustahimili taarifa hizo za msiba na kuzimia kwani alikuwa
mtu wake wa karibu sana.
Alipotafutwa na paparazi wetu mara baada ya kutoka hospitali juzi, Koleta alifunguka:
“Kuambiana alikuwa mtu wangu sana, nilishindwa kabisa kuhimili kifo chake na kama unakumbuka ndiye ambaye nilianza kuigiza naye filamu yake ya kwanza ya Sauti ya Manka.”
“Kuambiana alikuwa mtu wangu sana, nilishindwa kabisa kuhimili kifo chake na kama unakumbuka ndiye ambaye nilianza kuigiza naye filamu yake ya kwanza ya Sauti ya Manka.”
No comments:
Post a Comment