Kituko
kingine cha tatu leo kinatoka Italia ambapo Jaji mmoja ameamua
kusimamisha kesi baada ya kuona wafanyakazi wawili wa Mahakama hiyo
wakifanya mapenzi kwenye chumba cha jirani wakati kesi ikiendelea.
Jaji
Anna Ivaldi alishtuka na kumuomba mwendesha mashtaka anyamaze baada ya
kuona tukio hilo ndani ya ofisi pembeni ya mahakama ambapo wawili hao
walidhani kioo kilichoua na tinted pembeni yao kisingeweza kumpa nafasi
mtu wa upande wa pili kuona kinachoendelea ndani.
Taarifa
kutoka kwenye Mahakama hiyo zinaamplfy kwamba mmoja kati ya wawili hao
anatambulika kuwa yuko kwenye ndoa na hii ni kwamujibu wa mmoja wa
wafanyakazi wa Mahakama.
Mmoja
kati ya waliokuwemo mahakamani amesema “wakili ndio kwanza alianza
kuzungumza, jaji akasikia kelele za mahaba na alipoangalia juu na kuona
miili miwili ikiwa uchi ilifanya kila mtu akatazama ambapo tuliona watu
wawili wakifanya mapenzi na inaonesha walikua hawajui kama wanaonekana
na wakati tunawatazama bado walikua wanaendeleza.
Kesi
ilisimamishwa na wawili hao waliondoshwa eneo hilo na kupata mshtuko
ambapo majina yao hayajatajwa huku mzungumzaji wa Genoa Court akisema
kesi imesimamishwa kwa muda na tukio hilo limeshashughulikiwa na
haitakuwa sawa kuzungumzia zaidi.
No comments:
Post a Comment