YULE mwanamke aliyejulikana kwa jina la Mariam
Manyata (57) ambaye aliandikwa kwenye gazeti hili Toleo Na. 838,
Aprili 15 hadi 21, mwaka huu ukurasa wa 15 kwa kichwa cha habari HUU
SI UJAUZITO JAMANI, TUMBO LIMEJAA MAJI, amefariki dunia.
Mwanamke huyo (pichani) alifariki dunia Mei 5, mwaka huu katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili Jengo la Mwaisela alipokuwa akikendelea
na matibabu.
Lengo la habari ile ya kusikitisha lilikuwa ni mwanamke huyo
kupata msaada baada ya kukosa fedha kwa ajili ya matibabu akiwa katika
hospitali hiyo.
Mariam alizikwa Mei 9, mwaka huu kwenye Kijiji cha Mlodaa, Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambako ndiko alikokuwa akiishi.
Mwili wake kutoka Dar ulisafirishwa na Umoja wa Chama cha Iringa -Mvumi ambapo wakazi wake wanaishi Dar.
Gazeti hili linatoa shukrani kwa Watanzania wote waliokuwa na nia ya kumsadia Mariam lakini Mungu amempenda zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment