Katika harakati za kutafuta mbinu bora za malezi mazuri kwa watoto
wake, Nyota wa muziki wa R&B wa nchini Marekani Tony Braxton
anafanya jitihada za kuwafundisha watoto wake usimamizi mzuri wa fedha
kwa kuwalipisha kodi ya kuishi katika nyumba yake kwa madai kuwa
anawafundisha maisha.
Braxton aliyewahi kutamba na vibao vikali kama Unbreak My Heart ni
mama wa watoto wawili wa kiume Denim mwenye umri wa miaka 12 na Diezel
mwenye miaka 11. Ingawa mafanikio yake makubwa kama mwanamuziki
yamesaidia kulea familia na kutoa mahitaji muhimu ya familia yake, Tony
ameanza utaratibu huo kwa watoto wake ili wajue thamani ya dola.
Katika mahojiano na kipindi cha Televisheni cha Queen Latifah nchini
Marekani, Braxton ameweka wazi kuwa watoto wake wanapata dola 10 na 12
kwa wiki ambapo mmoja humlipa dola mbili na mwingine tatu ambapo
wanatakiwa pia kulipia senti 75 kwa ajili ya gesi na umeme.
Wakati wazazi wengine wakiwa hawafanyi kitendo hicho, Kwa upande wake
Braxton anasisitiza kuwa ana matumaini kuwa mafunzo hayo ya matumizi
mazuri ya pesa kwa watoto wake yanawaandaa vyema katika maisha yao ya
baadae.
Braxton amefafanua kuwa kwa kufanya watoto wake watajua thamani ya
fedha na watakapokuwa wakubwa watahitajika kulipa bili zote kwa wakati
kwa kuwa wamezoea utaratibu huo.
No comments:
Post a Comment