RB namba STK//RB/4457/2014 -KUTUMIA LUGHA YA MATUSI inawahusu
wanandoa waliodumu kwa zaidi ya miaka 10, waliofunga ndoa kwa mbwembwe
nyingi, Nyange na Ruth kisa kikielezwa kuwa ni ticha anayedaiwa kuvunja
utatu huo mtakatifu, Ijumaa lina kisa na mkasa.
Habari zilieleza kwamba wahusika ni wakazi wa Pugu, Dar.
Kwa
mujibu wa habari za mtaani wanakoishi wawili hao wanadaiwa kufikishana
kwenye Kituo cha Polisi cha Sitaki-Shari, Dar baada ya mke kumfungulia
mumewe jalada hilo la kesi baada ya ndoa yao kupigwa kimbunga.
Kuna madai mazito kwamba mke anamlalamikia mumewe kumjali zaidi
hawara ambaye anadaiwa naye ni mke wa mtu akiwa ni mtumishi wa serikali
yaani mwalimu.
Akisimulia kila kitu kwa gazeti hili, Ruth aliyefukuzwa na mumewe
alisema kwamba utatu wake na mumewe uliingia mchanga kitambo bila yeye
kujua chanzo kwani hakuwa mfuatiliaji lakini baada ya kufuatilia
alibaini kuwa kuna mchepuko kwenye ndoa yake.
“Nilikuwa sijui ndoa yangu inachezewa na mtu gani, baadaye nilinasa
mawasiliano ya simu ilibidi nifanye uchunguzi wa kina ili kumbaini
mbaya wangu kitu ambacho nilikifanikisha kwa kiasi kikubwa alisema
Ruth.
Kutokana na hali hiyo mume wake aliendelea kufanya manyanyaso huku
akiendelea na mawasilino ya karibu na mwalimu huyo ambaye pia ni mke
wa mtu.
Mama huyo alidai kuwa mume wake amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na
mke wa mtu huyo ambaye ni huyo mwalimu na kusababisha pia ndoa yake
kuingia matatani.
Ninachokizungumza ni sahihi kwa sababu hata siku ninamkamata mume
wangu alikuwa kwa mwalimu huyo ambapo siku hiyo alimpelekea sukari na
matumizi mengine hali iliyosababisha timbwili kubwa, nilifanikiwa
kumnyang’anya mume wangu ile mizigo aliyokuwa amepeleka kwa huyo
mwanamke.
Mpaka sasa tunavyoongea huyo mwalimu ndoa yake iko matatani kutokana
na jeuri aliyokuwa akipewa na mume wangu maana inadaiwa kuwa hata
nyumba anayoishi mume wangu ndiye mlipa kodi.
Katika kikao kilichokaa shuleni mwaka jana kwa mwalimu huyo
kuhusiana na tukio hilo, mwalimu huyo alikiri kuwa na mahusiano na mume
wangu lakini aliahidi kuachana naye mbele ya kikao hicho, cha
kushangaza hadi leo bado wanaendelea na mahusiano.
Alipoulizwa mwalimu huyo ambaye ametajwa kwa jina moja la Catherine
Rokio Mayengo au Elizabeth Rokio Mayengo kwa njia ya simu kuhusiana
na sakata hilo alimwambia mwandishi wetu kuwa namuuliza kama nani.
Mwandishi alijitambulisha na kumwambia anataka kujua hayo yanayosemwa na Ruth Nyange mwalimu yana ukweli gani.
Mwalimu huyo alisema hawezi kuongea na udaku hivyo kama ni kuandikwa habari hiyo iandikwa kadiri mwandishi anavyoweza.
Mbali na hilo mwalimu huyo alimwandikia ujumbe mwandishi wetu
unaosema kuwa yeye anamilikiwa na serikali na haogopi kitu au jambo
lolote na anajiamini na anapenda watu wanaotumwa kama mwandishi waende
Stakishari.
Mwandishi wetu alifanikiwa kumpata mume wa mwalimu huyo ambaye
alijitambulisha kwa jina la Evansi na kukiri kuwa huyo ni mke wake wa
ndoa lakini hawako naye kwa muda huu.
Kuhusu mke wake kuwa na uhusiano na mtu mwingie, alisema inawezekana
maana alianza ukorofi na kuamua kwenda kupanga lakini taarifa zilizopo
amepangishiwa na mwanaume ambaye yeye hamjui.
Huyo mwalimu ni mke wangu wa ndoa hata mimi ninashangaa kuacha ndoa
yake na kwenda kupanga na kuacha watoto wawili ambao tumezaa wote
wakiwa wanateseka kwa kukosa mapenzi ya mama.
Mwandishi wa habari hii alifanya kila mbinu ya kukutana na
mlalamikiwa ambaye ni Grey Godwin Nyange lakini ilishindikana na
kujibu kwa njia ya simu kuwa habari anazoambiwa hazifahamu labda huyo
aliysema hayo ndiye anayejua undani wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment