Vijana hao wanaonekana wakiimba na kucheza hadi juu ya paa la nyumba.
Kikundi hicho kimefunguliwa mashitaka kwa madai kuwa kimekiuka maadili ya Iran kwa kuwa pamoja na mambo mengine, wanawake walioonekana kwenye video hiyo wamevaa mavazi ya kawaida ambayo hayafuniki kichwani hadi viganja vya miguu.
Kitendo hicho ni kinyume cha sheria ya mavazi ya nchi hiyo inayowataka wanawake wote kuvaa nguo zinazofunika kichwa hadi viganjani.
Vijana hao walipoulizwa, wamedai kuwa walidanganywa na mtu mmoja kuwa amepewa kibali cha kushuti video hiyo na kwamba ilikuwa sehemu ya usaili wa kuigiza filamu.
Polisi wa Tehran wamesisitiza kuwa video hiyo imekiuka maadili ya jamii ya Iran na kwamba lazima sheria ifuate mkondo.
Nae Pharrell Williams ameoneshwa kushangazwa na hatua ya polisi wa Tehran na kupitia Facebook ameandika, “Yaani siamini kama watoto hawa walikamatwa kwa kujaribu kueneza furaha.”
Watu mbalimbali wameanza kupinga uamuzi huo wa Iran na wameanzisha harakati za kupinga kitendo hicho kupitia mitandao kwa hash tah
No comments:
Post a Comment