Wadada
wengi wamekuwa wanahamu sana ya kujua sana,kama mwanaume aliyenaye
ataenda kumuoa au anapoteza muda wake tu,hii imepelekea hata wadada
wengi ambao wako kwenye msako wa kutafuta wenzi wao wa maisha,kuwa na
wapenzi hata zaidi ya wawili,kwa sababu tuhawana uhakika kati ya yupi
anaweza kuwa wa maisha yake,basi uonapo viashiria hivi ujue kuwa
mwanaume huyo yupo serious na wewe.
#1.Anajisifia kila saa kuhusu wewe kwa marafiki zake..
kama kimetokea kitu kizuri au amefanikiwa kufanya jambo fulani
kazini,hawezi kujizuia kukutaja kwa marafiki zake kuwa bila wewe vyote
visingewezekana,sababu ni wanaume wachache sana wanaweza kuwataja
wapenzi wao mbele ya marafiki zao mbali zaidi na yakusifia yenyewe.
#2. Anakufanyia vitu usivyotarajia—mfano
kwa wale wanaofanikiwa kupata kazi mbali na mkoa,sana sana kazi hizi za
kupangiwa na serikali,utakuta mwanaume anatumia muda mwingi kila
akipata,kuja kukutembelea,tena wengine unakuta anahama kabisa kwa muda
kuja kukaa na wewe popote pale utakapokuwa.
#3. Wote mnakuwa na mtazamo unaofanana. Kwa mwanaume anayekujali na ambaye yuko teyari kukaa na wewe kwa muda mrefu,utakuta mapendekezo yako mengi hasa yale yenye umuhimu, wote mnakubaliana mara moja bila hata ya ubishani wowote ule,anaepuka sana kukuudhi au kukufanya ukasirike.
#4.Hata kama mmekaa miaka toka mwanzo wa mahusiano yenu unakuta anafanya mambo yale ya wapenzi wachanga,kama
kukufungulia mlango mara kwa mara,kukushika mkono mtembeapo,kukuambia
anakupenda mara kwa mara na vitu kama hivyo,hapa ujue kuwa hayuko teyari
kukupoteza,na zaidi unakuta hayuko teyari kukuacha uende mahali peke yako ,unakuta anakuuliza kama utapenda kusindikizwa.
#5. Hatajaribu kukubadili.
Kwa kila jambo ufanyalo,mara nyingi hutakuta kukaa ukamuona anajaribu
kukubadili sababu amekupenda kama ulivyo,na yuko teyari kuishi na
mapungufu yako ulionayo..
#6. Anajali marafiki zako. Wanaume
wengi wanajua kuwa marafiki zako wakaribu ndio ulimwengu wako na hayuko
teyari kukuambia uachane nao,zaidi utakuta anajitahidi kuwa karibu
nao,hata kama imepita muda hajasikia kuhusu rafiki yako anaweza
kukuuliza vipi anaendeleaje au yuko wapi siku hizi,ni njia moja wapo
yakujua kuwa huyu mwanaume kweli ana malengo makubwa na mimi.
#7. Mnaweza kustahimili mapenzi ya mbali bila yakukata tamaa.
Kwa mwanaume anayekujali na kutarajia kukuita mke siku moja,mapenzi ya
mbali kwake siyo tatizo,yuko radhi kukusubiri kwa muda wowote ule hadi
pale utakaporejea bila hata yakukusaliti na mwanamke mwingine,anakupigia
kila siku,mnachat sana, hii yote ni kwa sababu sehemu kubwa ya maisha
yake ni wewe, bila kujali upo umbali gani.
#8. Yeye ni mtu wa pekee wa kumwendea unapokuwa na tatizo,au
kitu chochote cha kuongea.Kuhusu kazini,kuhusu rafiki yako au chochote
kile kinachokusumbua kichwani ,unakuwa upo free kuongea naye vitu vyote
ambavyo awali ulikuwa free kuongea na wazazi wako au marafiki wako
wakubwa,na yuko radhi kukaa na kukusikiliza chochote utakacho
mwambia,sababu mwisho wa siku anataka uwe na furaha
#9. Unaweza kulia mbele yake bila kujisikia aibu.kuna
ile hali yakumzoea mpenzi wako na kumzoea kama best friend wako,hadi
kufanya nae vitu ambavyo hutaona aibu kufanya yake,hutaona aibu akikuona
ukifanya,zaidi unajisikia free hata kulia mbele yake sababu,
anakusikiliza na kukubembeleza kwa sababu unajua kuwa mpenzi wako hata
ku-judge .
#10.Anakuwa karibu sana na ndugu zako.kwa
mwanaume mwenye malengo ya mbali na wewe, utamkuta anajenga mahusiano
ya mapema na ndugu zako wa karibu,anamuita baba ua mama, wazazi wako
kama uwaitapo wewe bila hata kujishtukia ,wengine utakuta hata kama
haupo anaweza kufanya birthday party ya mdogo wako au ndugu yako yeyote
yule.
No comments:
Post a Comment