Michuano
ya kombe la dunia imeendelea kuonyesha ukubwa wake kwa kuteka kila
habari kuu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, mabilioni ya
watu duniani kote wakiwemo mastaa wakubwa wa kitaifa na kimataifa
wanafuatilia michuano hii ambayo ndio mikubwa kabisa katika soka
duniani.
Mmoja wa mastaa wa kibongo ambaye ameonyesha kufuatilia michuano hii
pamoja na wachezaji shiriki ni Jokate Mwegelo, ambaye mtangazaji wa TV,
muigizaji na mmiliki wa lebo mavazi na fashion kiujumla ya Kidoti.
Tangu kuanza kwa michuano hiyo Jokate amekuwa akiposti posti tofauti
kuhusiana na michuano hiyo, huku akionyesha namna anavyomkubali
mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo, mshambuliaji wa Real Madrid
na timu ya taifa ya Ureno inayoshiriki kwenye kombe la dunia mwaka huu.
“Ronaldo ni mchezaji mzuri, anajituma uwanjani na anafunga magoli
akiisadia timu anazochezea. Ana nidhamu ya kazi yake na akiifanya
anaifanya kiuhakika na ndio maana tangu akiwa Manchester United
nikajikuta namshabikia. Pamoja na hayo kitu kingine ambacho kinanifanya
kumkubali Ronnie, ni namna ambavyo anajitoa kusaidia watu wasiojiweza,
kama tulivyosikia juzi ametoa kiasi cha zaidi ya millioni 100 za
kitanzania kusaidia matibabu ya mtoto aliyekuwa na matatizo fuvu la
ubongo kujaa damu.”
Akizungumzia
michuano ya kombe la dunia, Kidoti alisema, “Kwenye michuano hii
nilikuwa nasapoti timu za Afrika lakini zinaniangusha, hazichezi vizuri.
Pia naisapoti Ureno kwa sababu ya nampenda Ronaldo, na Brazil pia
nawapenda wanacheza vizuri hasa yule Neymar. Van Persie pia namkubali,
lile goli alilofunga dhidi ya Spain kwa kichwa, aisee ni moja ya magoli
bora kabisa.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment