Mabaki ya magari katika shambulio la Mpeketoni.
WATU watano
wamepoteza maisha baada ya shambulio lililotokea usiku wa kuamkia leo
katika kijiji cha Pandanguo huko Witu wilayani Lamu nchini Kenya
kilometa 30 kutoka Mpeketoni yalipotokea mauaji ya watu zaidi ya 60 wiki
iliyopita.
Polisi wamesema kuwa waliouawa ni kutoka jamii mbalimbali.
Mkuu wa
Polisi nchini Kenya, David Kimaiyo amesema kuwa washambuliaji walivamia
kijiji cha Pandanguo na kuua takribani watu watano.
"Bado tunawasaka waliohusika na shambulio hili, habari zaidi zitatolewa baadaye," alisema Kimaiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment