BAADA A KIMYA CHA MUDA MREFU, ROSE MUHANDO AIBUKIA KWENYE FACEBOOK

Rose Muhando aibuka na ‘Facebook’
MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando, ameibuka na wimbo mpya uitwao ‘Facebook’.
Akizungumza na gazeti hili, Muhando alisema ana imani wimbo huo utakuwa kivutio kikubwa kwa jamii, hasa vijana kwa sababu una ujumbe mzuri ambao utagusa wengi.
“Sitaki kuwaambia nimeimba nini, lakini ‘Facebook’ ni wimbo mzuri na mashabiki wangu naamini wanatambua kwamba mimi si mtu wa masihara ninapotunga kazi zangu,” alitamba mwimbaji huyo.
Alieleza kuwa wimbo huo utakuwa katika albamu yake mpya iitwayo
‘Kamata Pindo la Yesu’ anayotarajia kuizindua jijini Dar es Salaam katika siku itakayotangazwa wakati wowote kuanzia leo.
Baadhi ya nyimbo zilizompa umaarufu msanii huyo ni pamoja na ‘Nipe Uvumilivu’, ‘Yerusalemu’, ‘Nakaza Mwendo’, ‘Kitimutimu’, ‘Mungu Wangu’, ‘Utamu wa Yesu’, ‘Jipange Sawasawa’ na ‘Vua Kiatu’, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger