Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa na mpenzi wake Siwema.
Tukio hilo la ajabu lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri
usiku wa kuamkia Juni 10, mwaka huu maeneo ya Kimara-Baruti, Dar ambako
staa huyo anaishi huku wahudhuriaji wakipombeka hadi kuzimika.Katika shughuli hiyo, kwa mara ya kwanza tangu walipodaiwa kumwagana na kurudiana, Nay alinaswa na yule Siwema wake.
Akizungumzia sherehe hiyo, Nay alisema hakuwa amepanga kuifanya lakini aliona ni kitu kizuri kukusanyika na baadhi ya ndugu, jamaa na rafiki zake wa karibu kwa ajili ya kusherehekea bethidei yake.
Alisema alishangazwa na kitendo cha ghafla kilichofanywa na baadhi ya ndugu cha kumwagia ndoo ya maji.
“Sikuwa na hili wala lile, ghafla tu wakati wameniita katika hadhara ili niweze kuwasalimia wageni na ndugu hao wa karibu, wakanizunguka na kuanza kunimiminia ndoo za maji,” alisema Nay wa Mitego.
Hata hivyo, pamoja na ndugu hao na marafiki kummwagia maji mengi tofauti na bethidei nyingine zinazofanyika, Nay hakukasirika na badala yake aliwashukuru kwa uwepo wao katika sherehe hiyo aliyokuwa akitimiza miaka 29.
Keki za bethidei.
“Nimefarijika sana kwa ndugu zangu kuja kujumuika na mimi kwenye
sherehe hii ya kuzaliwa kwangu ingawa wamenishtusha. “Pia baada ya
kuwaona wakinimwangia ndoo za maji jambo ambalo sikulitarajia kabisa
kwani nimelowesha vitu vyangu, ila kwa kuwa ni siku yangu ya kuzaliwa,
sijutii, nafurahia sherehe hii.“Namshukuru sana mpenzi wangu Siwema kwa kujumuika na marafiki zangu kusherehekea tukio hili ambalo ni la kipekee kwangu, kikubwa zaidi namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia uzima na afya tele tangu kuzaliwa hadi leo,” alisema Nay wa Mitego.
Utamaduni wa kumwagiana vinywaji au maji kwenye sherehe za bethidei umekua kwa kasi Bongo ambapo umekopiwa kutoka nchi za nje kama ilivyo suala la mavazi.
No comments:
Post a Comment