HUSNA WA BONGO MOVIE YUPO TAYARI KUOLEWA LAKINI SI NA MASIKINI ANATAKA MTU MWENYE PESA ZAKE

Husna Chobis
MWIGIZAJI wa kike wa filamu Bongo Husna Chobis 'Awena' amesema kuwa baada kurudi katika biashara zake nje ya nchi yupo tayari kuolewa lakini kwa mtu mwenye fedha na si mbabaishaji ambaye hawezi hata kumiliki Bajaji hamuitaji, lakini kwa wale ambao wanaona wanajiweza kuwa wachapakazi na wanapata fedha ya kubadilisha mboga.


"Kuzaliwa katika familia ya kimaskini ni bahati mbaya, lakini kuchagua mume maskini ni uzembe na haustaili msamaha, ukitembea unajifunza mambo ya mastaa wa Ulaya wanavyoishi wanapotaka kuolewa wanatafuta wanaokwenda nao kimaslahi, hata mimi nahitaji mtu wa kueleweka na kipato pia,"anasema Husna.

Mwigizaji huyo aliyejizolea umaarufu katika filamu za kiasili hasa filamu ya "Ndase", anasema moja ya matatizo ya ndoa za kitanzania au kiafrika ni kukosa uchaguzi na kuingia katika uhusiano wa kupotezeana muda kisha kutengana kutokana na kuwa uzembe wa kukosa maamuzi kutoka kwa wanawake wengi

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger