Blandina Chagula 'Johari' ambaye ni mmoja wa washiriki wa filamu mpya ya Wrong Hope amewaponda wasanii wa filamu wanaokubali kukatishwa viuno mbele ya hadhara na kueleza kwamba kamwe kwa upande wake hawezi kufanya jambo hilo hata kwa malipo namna gani...!!!
"Siwezi
kujidhalilisha mbele ya umati kwa kukata kiuno, ni ulimbukeni
tu kukata viuno mbele ya watu, labda niwe nimelewa kiasi cha
kutojitambua ndo naweza kufanya madudu kama hayo," alisema Johari.
Aidha,
Johari alisema kuwa kuna umuhimu kwa wasanii wa filamu
kujitambua na kufanya mambo ya maana kwa jamii kuliko
kujigeuza kituko na kufanya mambo ya ajabu.
Mrembo
huyo alihitimisha kwa kuwaomba mashabiki wake waipokee kwa
mikono miwili filamu yake mpya ya Wrong Hope itakayotoka mwezi
ujao ambapo ndani yake yumo Mohammed Nurdin 'Chekbudi' na
marehemu Sheila Haule 'Recho'.
No comments:
Post a Comment