Meriam
akiwa na mwanaye Maya, kushoto ni mumewe Daniel Wani aliyempakata mtoto
wao wa kiume Martin na wadau waliopigania mama huyo kuachiwa huru kabla
ya kukamatwa tena leo.
MWANAMKE Meriam Ibrahim aliyeachiwa huru jana baada ya kuhukumiwa
kifo kwa kosa la kuolewa na mwanamume mkristo na kukana dini ya
kiisilamu amekamatwa tena akiwa na mumewe pamoja na watoto wawili katika
uwanja wa ndege mjini Khartoum, Sudan.Meriam amekamatwa na watu takribani 40 waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia ikiwa ni masaa 24 baada ya kuachiwa huru kutokana na uamuzi wa mahakama ya rufaa.
Inadaiwa kuwa Meriam aliyejifungulia jela alikuwa anajiandaa kuondoka nchini Sudan pamoja na familia yake.
No comments:
Post a Comment