Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 19
amekutwa amening’inizwa juu ya mti katika kijiji kimoja Kaskazini mwa
India, likiwa ni tukio la tatu kutokea ndani ya wiki moja katika Jimbo
la Uttar Pradesh.
Mwili wa mwanamke huyo umekutwa katika
eneo la Moradabad ambapo familia yake imewaambia polisi kuwa alibakwa
huku uchunguzi wa madaktari ukiendelea kufanyika.
Mwanamke mwingine alikutwa amening’inizwa juu ya mti katika Jimbo la Uttar Pradesh siku ya Jumatano.
Mwezi uliopita mabinti wawili wadogo
walibakwa na kundi la watu katika mazingira kama hayo na kuibua
maandamano ya hisia kali nchini India.
Siku ya Jumatano, mwanamke mwenye umri wa miaka 44 nae alikutwa amening’inizwa juu ya mti katika eneo la Bahraich.
Polisi wamesema kuwa alikuwa akipatiwa
vitisho na wanakijiji kwa kuuza pombe katika eneo hilo na familia yake
ilifungulia kesi watu watano kuhusiana na kifo hicho.
No comments:
Post a Comment