SERIKALI
imewataka Watanzania kununua simu zenye viwango kwa kuwa utafiti
uliofanywa na taasisi mbalimbali za afya duniani, umebaini kuwa mtumiaji
akizungumza kwa simu kwa muda mrefu, anapata madhara.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga, alisema hayo jana
alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Chonga, Haroub Mohamed Shamis
(CUF).
Chonga
katika swali lake alisema kwa kuwa imebaini kuwa utumiaji wa simu za
mkononi kwa zaidi ya dakika sita una madhara kwa afya za watumiaji hasa
wanapoongea na simu kwa zaidi ya dakika sita, Serikali ieleze inawalinda
vipi watumiaji hao.
Akijibu
swali hilo, Kitwanga alisema mawasiliano ya simu za mkononi
husafirishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa kupitia mawimbi ya
redio ambayo yanazalishwa na umeme.
Alisema
mawaimbi hayo katika hali ya kawaida yamethibitishwa kitaalamu kuwa
yako katika kiwango cha chini na hivyo kutokuwa na madhara na binadamu.
Alifafanua
kuwa pamoja na kuthibitisha huko, taasisi mbalimbali za kiafya duniani
zimebaini kuwa mawimbi hayo ya simu yana madhara pale mtumiaji
anapoongea kwa muda mrefu na hasa kwa kutumia zenye ubora ulio chini ya
viwango.
Ili
kulinda afya za watumiaji, Kitwanga alisema Serikali kupitia mamlaka
zake mbalimbali za udhibiti wa mawasiliano na viwango, inaendelea na
jitihada za kuelimisha wananchi kuhusu madhara hayo yanayoweza
kujitokeza kutokana na kuongea muda mrefu.
Pia
alisema Serikali inaendelea kuhakikisha bidhaa za simu zinazoingizwa
nchini zinakuwa na ubora unaotakkiwa pamoja na uwezo wa kumkinga
mtumiaji na madhara yanayoweza kujitokeza.
Aliwataka
wananchi kutumia simu za mkononi zenye ubora unaokubalika pamoja na
kushirikiana na Serikali katika kupambana na wafanyabiashara wanaoingiza
bidhaa za simu za mkononi zilizo chini ya ubora.
No comments:
Post a Comment