HII
ni kali lakini haikuwahi kuandikwa, staa wa Bongo Fleva, Ally Timbulo
alinusurika kuuawa baada ya kubainika kuwa anatembea na mke wa mtu na
mumewe kumsaka kwa udi na uvumba akiwa na bastola mkononi.
Akitema cheche na Untold, Timbulo alisema, katika maisha yake
hakuwahi kufikiria kutoka kimapenzi na mtu ambaye yupo kwenye ndoa,
isipokuwa mwanadada huyo ambaye anafanya kazi serikalini (jina kapuni)
alionesha upendo wa dhati kwake pamoja na kumgharamia kwa kila
alichohitaji.
“Hakuwahi kuniambia kama ni mke wa mtu maana nilionana naye muda
wowote nilipomuhitaji pia aliniganda vibaya mno na alikuwa tayari
nimuoe, kumbe mumewe alikuwa ameshapata taarifa kuwa najiachia na mkewe,
akanitafuta kwa njia ya simu na kunionya kuwa nikiendelea ataniua kwa
bastola,” alisema Timbulo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment