Dunia inahesabu masaa kabla ya kuanza kushuhudia faina za kombe la dunia
nchini Brazil huku kila timu ikijifua zaidi nchini humo huku usalama
ukiwa umepigiwa msitari na jeshi la Brazil.
Ulinzi mkali wa jeshi
unaousindikiza msafara wa timu hiyo popote uendapo uligeuka kero na
kikwazo kwa wenyeji wa miji ya Brazili itakayoshuhudia mechi za fainali
hizo zikichezwa.
Mjini Rio de Janeiro hali imekua ngumu kwa wakazi wa mji huo hususan
inapofika wakati timu zinapokwenda katika viwanja vya kufanya mazoezi ya
kujiandaa na michezo ya kombe la dunia itakayowakabili kuanzia siku ya
Al-khamisi ya wiki hii.
Jana wakazi wa jiji hilo walilazimika kusubiri kwa dakika 15 wakiwa
barabarani kwa ajili ya kupisha msafara wa timu ya taifa ya Uingereza
ambayo imepangiwa kufanya mazoezi kwenye kambi ya jeshi katika eneo la
Urca.
Kimbembe cha kusubiri kwa muda huyo wakiwa katika foleni
kilisababishwa na mshambuliaji wa klabu ya Everton Ross Barkley, ambae
almanusura aachwe hotolini baada ya kushindwa kwenda na muda wa
kujiandaa kabla ya kuingia kwenye basi kwa ajili ya kwenda mazoezini.
Tayari
wachezaji wenzake walikuwa wameshaingia kwenye basi na msafara ukataka
kuanza lakini ikabainika Ross Barkley hayupo garini, hivyo iliwalazimu
maafisa wa timu ya taifa ya Uingereza kuwaomba walinzi wa kambi yao
kufanya subra ambayo ilisababisha foleni kubwa.
No comments:
Post a Comment