Ilisemekana kwamba wakati hayo yakiendelea, Mbasha alikuwa nyuma ya nondo za Mahabusu ya Keko jijini Dar es Salaam ambako alishikiliwa.
Kwa mujibu wa mtu aliyeambatana na Mbasha alipopata dhamana dhidi ya kesi yake inayomkabili ya ubakaji wa shemejiye mwenye umri wa miaka 17, alipofika nyumbani kwake Tabata-Kimanga, Dar alipigwa butwaa kukuta hakuna vitu ndani!
Habari zilidai kwamba alipowauliza majirani kama walimuona mtu akiingia ndani walimwambia mkewe (Flora) ndiye alikuwa akiingia na kutoka mara kwa mara.
Ilielezwa kuwa vitu hivyo vilihamishwa Juni 16 ambapo Mbasha alitoka mahabusu Juni 17, yaani siku moja tu.
KITANDA CHA BEI MBAYA
Baadhi ya vitu vilivyodaiwa kuchukuliwa nyumbani hapo ni kitanda cha bei mbaya walichokuwa wakilalia kwenye chumba cha baba na mama huku akimwachia neti ikiwa inaning’inia.
SUTI ZA MAREKANI
Vingine ni makochi huku akibakisha sofa ndogo ya mtu mmoja, vitu vyote jikoni na nguo (suti za bei mbaya, walizonunua wakati wakiwa Marekani).
Pia alidaiwa kukomba vile vidani vyote vya dhahabu.
Mwandishi wa Global, Haruni Sanchawa akipata undani wa habari kutoka kwa baba mzazi wa Emmanuel Mbasha, Mzee Maneno.
ZAIDI YA MIL. 13Ukiacha zile hati za nyumba, viwanja na mashamba, gharama ya vitu vyote vilivyochukuliwa ndani ni zaidi ya Sh. milioni 13 za Kitanzania (kama zile ambazo Wema Isaac Sepetu alizomlipia Kajala Masanja asiende jela).
AMWAGA CHOZI
Baada ya kukutana na mazingira ya aina hiyo, lilikuwa ni pigo lingine zito kwa Mbasha ambaye alijikuta akimwaga chozi kwa mara nyingine kwa sababu ya mkewe Flora aliyedumu naye katika ndoa kwa takriban miaka 12.
Ilidaiwa kuwa, Mbasha aliumia kupita kiasi huku akiomba Watanzania waone ubaya aliotendewa.
AMANI LAPEKUWA CHUMBA HADI CHUMBA
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Amani lilifika nyumbani hapo ambapo lilipata mwanya wa kuingia ndani ya nyumba hiyo kisha kupekuwa chumba hadi chumba na kujionea kulivyokuwa kweupe huku madirishani mapazia yakiendelea kubembea kwa upepo mkali uliopo Dar kwa sasa.
Kimuonekano, nyumba hiyo ilikuwa kama kuna familia ilihama hivyo inahitaji kupangishwa au kuhamiwa na mwingine.
MBASHA ANASEMAJE?
Alipotafutwa Mbasha kuzungumzia ishu hiyo alikiri kukuta hali hiyo nyumbani kwake baada ya kupata dhamana.
“Nilipofika nyumbani kwangu nilikuta ufunguo wa nyumba kwa majirani. Niliwauliza kama kulikuwa na mtu anaingia nyumbani nikaambiwa ni Flora. Kama mnavyoona kuna vitu vingi vya ndani havipo,” alisema Mbasha.
Alipoulizwa kama ana uhakika kuwa mhusika ni Flora, Mbasha alisema yeye alikuta nyumba nyeupe.
Jitihada za kumpata Flora hazikuzaa matunda kwani simu yake ya kiganjani haikuwa hewani juzi Jumanne mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni.
TUMEFIKAJE HAPA?
Kabla ya Mbasha kukabiliwa na kesi hiyo ya madai ya ubakaji wa ndugu wa Flora, Mei 23 na 25, mwaka huu, tayari kulikuwa na mgogoro wa ndoa. Flora alishaondoka nyumbani na kwenda kuishi hotelini maeneo ya Sinza jijini Dar.
MSIKILIZE NA FLORA MBASHA ALIVYOFUNGUKA KUHUSU SAKATA LA MUMEWE ALIPOONGEA NA GLOBAL TV ONLINE
Wakati kesi ya ubakaji ikiendelea kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar huku Mbasha akiwa nje kwa dhamana, kuna jitihada zinazoendelea ili warudiane kwani kashfa hiyo inashusha upako wa huduma yao kwa jamii huku wote wakiwa tayari kwa suluhu.
No comments:
Post a Comment