Katika
hali isiyotarajiwa, mchumba wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’,
Wema Sepetu na aliyewahi kuwa mchumba wa msanii huyo, Penniel Mungilwa
‘Penny’ walikutana studio na kila mmoja akamkwepa mwenzake.
Tukio
hilo lilitokea juzikati maeneo ya Posta, jijini Dar katika Studio za
Amaya ambayo ni saluni inayotumika kurekodia vipindi mbalimbali vya
Mkasi vinavyorushwa kupitia Runinga ya EATV.
Kwa
mujibu wa chanzo makini, mwigizaji Aunt Ezekiel alialikwa na mtangazaji
wa kipindi hicho, Salama Jabir kwenda kufanya mahojiano, akaambatana na
shosti wake Wema ndipo ghafla wakakutana na Penny ambaye naye alialikwa
kwa wakati wake.
Chanzo
kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya Aunt na Wema kufika studio hapo,
Salama aliwakaribisha na wakaanza kurekodi kipindi hicho, lakini
walipokuwa wakiendelea na mahojiano, Penny naye aliwasili bila kujua
kama Wema alikuwepo. “Penny alipofika alizama ndani na kukutana na
Salama ambaye alimwambia kuwa kuna watu wanatoka ndani muda si mrefu
hivyo wakati bado wanaongea,
Wema
na Aunt walitoka studio ambapo Penny alikimbilia kwenye gari lake
kukwepa kuonana na Wema ambaye pia alionekana kutotaka kuonana na
Penny,” kilisema chanzo na kuongeza:
“Kwa
kuwa Wema naye alimuona kwa mbali Penny, alimtaka Aunt waingie kwenye
gari fastafasta na kuondoka eneo hilo.” Mapaparazi wetu baada ya
kuunyaka mchongo huo, walimtafuta Penny ili kumsikia anazungumziaje ishu
hiyo.
Alipopatikana,
alijibu hivi: “Mimi sikumkimbia Wema na itambulike kuwa wakati naenda
pale sikujua kama Wema alikuwepo hivyo nilifika na kusubiria muda wangu
wa mahojiano nikiwa ndani ya gari, sikuwa na haja ya kujua Wema yupo ama
la.”
Jitihada
za kumpata Wema hazikuzaa matunda lakini alipotafutwa Aunt Ezekiel,
alitiririka: “Nilimuona Penny kweli pale studio ingawa mwanzo
nilitahamaki maana sikujua kama naye alikuwa akisubiria tutoke aingie
kwenye kipindi ila Salama alinishtua sana baada ya kusema kabla
hatujatoka ndani tusubiri aandae uwanja wa ngumi, alitania.”
Wema
na Penny wanadaiwa kuwa picha haziendi baada ya Wema kumtuhumu Penny
ambaye alikuwa rafiki yake kuwa alimwibia Diamond wake kabla
hawajamwagana na kurejea tena mikononi mwake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment