'Beautiful Onyinye' na kipenzi cha Diamond, Wema Sepetu sasa ni mjamzito. Baada ya misukosuko ya muda mrefu ikiwemo kuporwa na wasichana wenzake penzi lake la Diamond, sasa Wema amepata kile alichokuwa akikililia kwa muda mrefu....
Chanzo
cha habari hii kutoka kwa marafiki wa Diamond kimedai kuwa
Wema amenasa ujauzito na kugundulika hivyo walipokuwa Afrika
Kusini kwenye tuzo za MTV-MAMA na kumfanya Diamond
achanganyikiwe kwa furaha....
Kwa
mujibu wa chanzo hicho, inadaiwa kuwa Diamond kwa sasa kawa
kama mtu aliyepagawa kwa furaha kutokana na taarifa hizo njema
na tayari ameshaanza maandalizi ya kijacho chake....
Kugundulika
kwa ujauzito wa Wema ni baada ya kuanza kujisikia vibaya
walipokuwa Afrika Kusini ikiwemo kichefuchefu na kizunguzungu
alipokuwa hotelini alipofikia na kulazimika kwenda hospitali kwa
uchunguzi zaidi....
Inasemekana
kuwa Wema alisindikizwa na Aunt Ezekiel kwenda hospitalini
waliyekuwa naye huko Afrika Kusini kumpa sapoti Diamond na
madaktari ndiyo waliomjuza kuwa anakiumbe tumboni cha wiki 7...
Taarifa
za madaktari hao zilimfanya Wema awe kama mwehu aliyepagawa
na kurudi hotelini kwa mumewe Diamond huku akiwa na tabasamu
ambalo hapo awali Diamond hakuwahi kuliona....
Inasemekana
kuwa mpaka sasa siyo Diamond wala Wema aliyewaambia wazazi
wake kuhusiana na mimba hiyo zaidi ya watu wa karibu wa
wawili hao waliowasindikiza Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment