TOFAUTI na mwaka jana ambapo msanii wa muziki wa dansi nchini,
Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ hakuweza kufunga, mwaka huu amesema
anafunga mwanzo mwisho mpaka mwezi mtukufu uishe.
Akistorisha na Ijumaa, Banza alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa mwaka
huu ameweza kufunga kwani mwaka jana alishindwa kufunga hata siku moja
kutokana na afya yake kutokuwa vizuri.
“Nashukuru mwaka huu naweza kufunga kwani mwaka jana nilishindwa, na
hivi niko nyumbani tu najipanga sijajua baada ya mfungo nitaenda kwenye
bendi au laa ila nataka nipumzike kwanza muziki,” alisema Banza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment