Dereva wa bodaboda aliyetambulika kwa jina la Abuu Athumani ambaye amenusa kifo baada ya kukwapua simu.
Tukio hilo la aina yake lilijiri majira ya asubuhi wikiendi iliyopita
maeneo ya Sinza-Mapambano, Dar ambapo kwa mujibu wa mashuhuda bodaboda
huyo alikuwa amempakiza mwenzake kisha kumfuatilia mrembo huyo kwa nyuma
wakati akitembea kwa miguu pembezoni mwa Barabara ya Shekilango.
Shuhuda huyo alisema kuwa alishangaa
kumuona yule jamaa aliyepakizwa akimkwapua mrembo huyo lakini kwa bahati
nzuri mmoja wa madereva wa Bajaj aliyekuwa karibu alimuona na
kumbananisha pembezoni mwa barabara na hatimaye kuingia mtaroni.Raia wakiitoa bodaboda kutoka mtaroni.
Ndani ya dakika sifuri, yule mkwapuaji alitoka nduki huku akimwacha bodaboda huyo aliyekiona cha moto. Zaituni Hamisi (kulia) aliyekwapuliwa simu yake na waendesha bodaboda.
Alisema ghafla umati ulijaa na kushuhudiwa akipewa kipondo cha kufa
mtu na wengine wakidai kuwa ni kawaida ya jamaa huyo kukwapua mikoba ya
watu.Baadhi ya watu walikuwa wakichanga fedha kwa ajili ya kununua
mafuta ya petroli ili wamchome moto bila kujali polisi aliyefika ambaye
alikuwa akijitahidi kutuliza ghasia hizo.Wakati akipewa kipigo, njemba huyo alikuwa akilalamika na kuwaomba wananchi wasimuue kwani amekoma na hatarudia tena.Hata hivyo, bodaboda huyo alinusurika baada ya polisi wa Kituo cha Kijitonyama (Mabatini) kufika eneo hilo kisha kumchukua jamaa huyo na mlalamikaji kwa ajili ya hatua za kisheria
No comments:
Post a Comment