Mtangazaji
wa kipindi cha mahaba kiitwacho Ala za Roho kupitia Radio Clouds FM,
Loveness Malinzi ‘Diva’ hivi karibuni alilazimika kuyaanika maungo yake
ya sehemu za mapaja kushuka chini baada ya kutakiwa kufanya hivyo na
mmoja wa mashabiki wake.
Kupitia
blog yake, Diva alidai kuwa siku za nyuma kuna mtu aliomba kuona sehemu
hizo za mwili wake hivyo baada ya kumbania sana ameamua kumtimizia haja
yake ili afurahi.
“Kuna
mtu alikuwa akidai hajawahi kuona miguu yangu iko ikoje na kwamba
nimekuwa nikionesha sehemu ya shingo tena kwa upande,leo nimeamua
kumfurahisha,”alisema Diva.
Sambamba
na maneno hayo, mtangazaji huyo alijifotoa picha zilizoocha wazi sehemu
kubwa ya mapaja yake kisha kuziweka kwenye ukurasa huo.
Diva
ni mtangazaji mwenye sauti ya kimahaba, yenye uwezo wa kumtoa nyoka
pangoni ambaye watu wengi wamekuwa na hamu ya kumuona jinsi alivyo kwani
wamezoea kumsikia redioni tu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment