DIAMOND AMLIZA MAMA’KE HADI KUMWAGA CHOZI KWA MASAA KADHAA

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amefanya tukio la kihistoria kiasi cha kumliza mama yake mzazi, Sanura Kassim ambaye alimwaga machozi kama mtoto mbele za watu.
Tukio la mama Diamond kumwaga machozi lilishuhudiwa na kamera za Amani, juzi Jumatatu, mishale ya saa mbili usiku nyumbani kwake, Sinza jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na ‘bethidei’ ya mama huyo.

...Mama Diamond akilia kwa furaha.
SAPRAIZI YA NGUVU
Waalikwa na mama huyo, wote walijua kuwa shughuli ilikuwa ni futari lakini kumbe nyuma ya pazia kulikuwa na tukio la kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mama huyo ambayo inadaiwa alikuwa hakumbuki.
Mmoja wa rafiki wa karibu na familia hiyo, kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, alisema kuwa hadi jioni, mama Diamond hakuwa akifahamu kuwa aliandaliwa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa.
Kilio kikiendelea.
“Mipango yote ilifanywa kwa siri mama Diamond hakujua kilichoendelea. Diamond akiwa Marekani alitoa maelekezo mama yake afanyiwe shughuli hiyo hata kama hayupo kwa sababu siku ya kuzaliwa haijirudii,” alisema rafiki huyo.
Wema na mama mkwe wake.
KILICHOMLIZA
Muda mfupi baada ya shughuli ya kufuturu kukamilika, mama Diamond alishangaa kusikia kwamba kulikuwa na jambo jingine la ziada katika siku hiyo. Alitolewa nje huku akiimbiwa ‘happy birthday’ ndipo alipogundua kilichokuwa kikiendelea.
Mara baada ya shampeni isiyo na kilevi kufunguliwa na waalikwa kupewa, meneja wa Diamond, Babu Tale na wapambe wengine walimuongoza mama huyo hadi kwenye gari aina ya Toyota Lexus Harrier na kuelezwa kuwa ni mali yake kuanzia muda huo tamko lililomshtua na kuanza kulia akiwa haamini alichosikia!Mama Diamond akilia huku kichwa kikiwa juu ya gari aliyopewa zawadi na mwanaye.
“Siamini macho yangu, siamini... asante sana mwanangu (Diamond), nakuombea kila kukicha mwanangu uwe na afya njema, unilee kwa upendo, asante Mungu,” alisikika mama Diamond akitamka kwa sauti iliyoambatana na kilio cha nguvu.
Muda huohuo akafunguliwa mlango na kuingia ndani ya gari hilo lililopambwa ndani kwa vitu kibao vya thamani.

Mama Diamond akiwa ndani ya gari aliyopewa zawadi.
WEMA, AUNT WAMBEMBELEZA
Machozi ya mama Diamond hayakukoma hata baada ya kushuka ndani ya gari, alionekana kuchanganyikiwa kama siyo kutoamini sapraizi ya mwanaye, ndipo Miss Tanzania 2006, aliye pia mchumba wa mwanaye,  Wema Sepetu na staa wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel walipovaa jukumu la kumtuliza.

Mastaa hao ambao ni mtu na shogaye, walimchukua mwanamke huyo na kwenda naye pembeni ambako walimsihi atulie na akubaliane na alichokiona kwani ndiyo ukweli wenyewe.
Juhudi zao zilizaa matunda, kwani muda mfupi baadaye mama Diamond alifuta machozi na kurudi katika hali yake ya kawaida ingawa alishindwa kuficha furaha yake.
Gari yenyewe ikionekana kwa mbele.
DIAMOND, WEMA NDOA LAZIMA!
Katika kuonesha kuwa sasa amekubali kwa dhati Wema awe mkwewe, mama Diamond aliapa lazima ahakikishe mwanaye anafunga ndoa na mlimbwende huyo.

“Hilo nataka mlijue kabisa. Nitafanya juu chini Diamond amuoe Wema maana ana roho nzuri sana. Niseme ukweli kuwa huyu msichana ndiye chaguo langu na wanaendana sana na mwanangu.
“Angalia wakiwa pamoja, mwanangu anapata mafanikio makubwa sana, nadhani nyota zao zinaendana hivyo sina pingamizi lolote. Ninachotaka ni kuhakikisha wanaoana,” alisema mama Diamond.

Keki iliyotolewa oda na Diamond iliyoandikwa ujumbe wake maalum.
THAMANI YA GARI
Akizungumzia thamani ya gari hilo, Babu Tale alisema ni shilingi 34,000,000 (milioni 34) ikiwa ni pamoja na mazagazaga mengine baada ya gari hilo kununuliwa.
“Hiyo milioni 34 ni pamoja na muziki unaouona ndani ya gari, hizi skrini tatu na mazagazaga mengine kama mnavyoona,” alisema Babu Tale huku akiwaonesha waandishi wetu.

Mama Diamond akikata keki maalum.
DIAMOND BONGO
Hadi tunakwenda mitamboni, Jumanne usiku, ilielezwa kuwa, Diamond alitarajiwa kutua jana Jumatano katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea Marekani alipokuwa kwenye kinyang’anyiro cha Tuzo za BET.

Habari kutoka ndani ya familia zilieleza kuwa, nyota huyo naye ameandaliwa sapraizi ya nguvu kutoka kwa kampani yake wakishirikiana na familia. “Wamejiandaa vya kutosha kumfanyia saprazi ya nguvu na yeye mara tu atakapotua Bongo. Wanafanya siri sana, haijajulikana atafanyiwa nini,” kilipasha chanzo chetu.
Mama Diamond, Bi. Sanura akimlisha keki 'mkwewe' Wema Sepetu katika sherehe yake ya kuzaliwa.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger