Dunia imekwisha! Jeshi la polisi mkoani hapa
linamshikilia mtoto wa miaka 14 (jina linahifadhiwa) anayesoma darasa la
sita kwa tuhuma nzito ya kuwalawiti wenzake watano kwa mpigo.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri katika Mtaa wa Twanga Pepeta
Kijiji cha Fulwe-Dindili Kata ya Mikese Wilaya ya Morogoro Vijijini
mkoani hapa ambapo dogo huyo alidaiwa kufanya tukio hilo ambalo ni gumzo
kwa sasa huku raia wenye hasira kali wakitishia kumshushia kipigo denti
huyo waliyempa jina la Babu Seya endapo ataachiwa na jeshi la polisi.
Mwanahabari wetu alifunga safari hadi kijijini hapo ambapo baadhi ya
wananchi waliohojiwa walidai kwamba dogo huyo alikuwa akiwalawiti
wenzake kwa kigezo cha kuwapanga kwenye mechi za mpira wa matambara.
lli kupata undani wa tukio hilo, mwanahabari wetu alifika nyumbani
kwa mtuhumiwa huyo na kukuta tayari jeshi la polisi lilifika
limeshamkamata.
Mjumbe wa serikali ya mtaa huo wa Twanga Pepeta
Kitwana Tupa alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanasubiri sheria
ichukue mkondo wake baada ya kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Morogoro, Leonald Poul.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment