MATESO! Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark
Productions inayoendesha shindano la kusaka vipaji vya muziki, Bongo
Star Search (BSS), Rita Paulsen ‘Madam’ amesimulia mateso aliyopitia
takriban mwaka sasa (siku 365) baada kuvunjika mguu mwaka jana alipopata
ajali ya gari katikati ya Jiji la Dar.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwenye mahojiano maalum hivi karibuni
aliponaswa na gongo linalomsaidia kutembea, Madam Rita alisema kwa
kusikitisha kwamba, baada ya kupata ajali alitibiwa kwenye Hospitali ya
Muhimbili lakini madaktari walimwambia aliteguka tu kumbe alikuwa
amevunjika mfupa.
“Nimepitia mateso makubwa. Mwaka jana baada ya kupata ajali na
kuvunjika mguu nilipopelekwa Muhimbili waliniambia nimeteguka tu, na
wakaamua kunifunga hogo ambalo baadaye walinifungua na kuniambia
nimepona,” alisimulia Madam Rita na kuongeza:
“Baada ya pale nilianza kujiachia hata niliposikia maumivu na
kuwaambia walisema niukanyagie tu kwamba hali hiyo ingebadilika kwa
sababu ulielekea kupona, kumbe nilikuwa nimevunjika kabisa mfupa na kama
ningejua siku nyingi hata nisingejiumiza kiasi hicho.
“Ujue baada ya kuambiwa hivyo, nilishangaa kuona maumivu yanazidi,
nikaamua kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuuangalia zaidi mguu
wangu kwa sababu maumivu yalikuwa yakiongezeka kila siku.
“Nilikwenda kwenye Hospitali ya Morning Site ya Afrika Kusini ambapo
nilifanyiwa upasuaji na kugundulika nilivunjika mfupa na kwamba tayari
nilipokuwa nikitembea ilikuwa ikipandiana.
“Ona sasa nilivyoteswa na mguu huu maana ajali nilipata mwaka jana na huu upasuaji nimefanyiwa mwaka huu Afrika Kusini.
“Kiukweli hospitali zetu saa nyingine zinatusababishia shida ambazo
siyo za lazima maana kama awali wangenifanyia upasuaji wakati nawaambia
ninaumia baada ya kunitoa hogo, basi leo ningekuwa nafanya shughuli
zangu.
“Naona bora pale Fame Centre (Dar) maana wao waligundua tatizo na
kunishauri kwenda Sauzi ambapo nimefanyiwa upasuaji na mguu unaelekea
kupona kwa sababu mwanzo nilikuwa natumia magongo mawili lakini ona leo
ninajikongoja kwa gongo moja ambalo nalo si muhimu sana sasa.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment