Moto mkubwa umeteketeza gereza la Nyakiriba lililoko Magharibi mwa Rwanda, katika wilaya ya Rubavu, karibu na mpaka wa DRC.
Tukio
hilo limeripotiwa kutokea Jumatatu (July 7) ambapo watu watatu
wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa vibaya kutokana na
moto huo.
Akiongea
na BBC, Mkuu wa wilaya ya Rubavu, Sheikh Hassan Bahame amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa waliopoteza maisha ni mahabusu
watatu na kwamba majeruhi 44 walikimbizwa hospitali kuu ya wilaya kupata
matibabu.
Amesema
ilikuwa vigumu kwa jeshi la zima moto kutekeleza kazi yake ipasavyo
kutokana na mazingira ya gereza hilo kuwa mlimani hali iliyopelekea vitu
vingi kuteketea.
Mkuu huyo wa wilaya alieleza kuwa bado hawajafahamu chanzo na thamani ya vitu vilivyoteketea katika tukio hilo.
Tukio hili linatokea mwezi mmoja baada ya gereza jingine la Muhanga kuteketea kwa moto katika jimbo lililopo kusini mwa Rwanda.
Tayari uchunguzi umeanza juu ya matukio hayo yote mawili.
No comments:
Post a Comment