MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya, Lucas Mkenda ‘Mr
Nice’ ameibuka na kufunguka kuwa siri ya kufilisika kwake ni kupenda
kwake sifa kutoka kwa wapambe na matumizi mabaya ya fedha alizokuwa
akiziingiza.
Akizungumza na paparazi wetu, Nice, aliyetamba kwa staili ya Takeu,
alisema wakati nyota yake ikiwa juu na kuingiza pesa nyingi kutokana na
kupata shoo nyingi, alikuwa akitembea na kundi la mabaunsa, akibadilisha
wanawake na kufanya matumizi makubwa yasiyo na lazima kwa lengo la
kutaka sifa.
“Enzi zangu nani asiyejua kuwa nilikuwa natembea na kundi la
mabaunsa, mademu na kila kumbi nikiingia basi kila mtu atajua kama Nice
yuko ndani lakini mwisho wa sifa zile ni nini? Si ndiyo zimenifikisha
hapa nilipo.
“Nilikuwa na kila aina ya kamati ya ufundi, mashehe, wachungaji na
maaskofu, wote walikuwa wangu, lakini kwa kuwa nilikuwa nataka sifa, dua
zao zilikuwa kazi bure kwa sababu nilikuwa mtu wa starehe,” alisema Mr.
Nice.
NENO LAKE KWA DIAMOND
Katika kile kinachoonekana
kama kumuonya staa wa sasa anayekimbiza katika Bongo Fleva, Abdul
Nasibu ‘Diamond’, alisema kwa kila ‘vurugu’ anayoifanya, yampasa
kumtazama yeye kama mfano halisi endapo ataendekeza maisha ya anasa na
kutaka sifa.
“Diamond kwa sasa anawika, anakubalika sana, ni kama ilivyokuwa
kwangu. Namsihi asijisahau. Maisha yanabadilika. Namtakia mema ndiyo
maana namshauri. Aachane na maisha ya kuwafurahisha watu, atengeneze
maisha yake yajayo.
“Kuna wakati muziki unakataa, hapo ndipo mawekezo yake yatakapomfanya
aendelee kuishi maisha bora bila muziki,” alisema Mr. Nice.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment