RACHEL NAYE ALISHWA UNGA, ANAWEZA KUWA KAMA RAY C, JUHUDI ZA HARAKA ZATAKIWA KUMNASUA

 
Kama  ilivyotokea  kwa  msanii nyota  wa  kike  wa  bongo  fleva, Rehema  Chalamira  'Ray C'  kuingizwa  katika  matumizi  ya  dawa  ya  kulevya  na  mtu  ambaye  alitokea  kumwamini  sana, ndivyo  ilivyotokea  sasa  kwa   msanii  anayefuata  nyendo  zake, Winfrida  Josephat 'Rachel'  ambapo  anadaiwa  kuvutishwa  unga  bila  kujua.... 

Kwa  mujibu  wa  chanzo  chetu  cha  karibu  na  msanii  huyo,Rachel  amewekewa  dawa  hizo  kupitia  kwenye  bangi  na  wakati  mwingine  kwenye  sigara hivyo  inakuwa  vigumu  kubaini  hila  iliyofanyika....

Habari  ambazo  tumezipata  zinadai  kwamba msanii  wa  kiume  nyota  wa  bongo  fleva ambaye  amewahi  kutuhumiwa  kutumia  dawa  za  kulevya  ndiye  anayemtengenezea  kokuteli  hiyo  inayotarajiwa  kumwangamiza  siku  za  usoni....

"Huyu  mtoto  ameshaanza  kutumia  dawa  za  kulevya.Huwezi  amini, hata  Ray C ameshapewa  taarifa,  hivyo  anamsaka  kuhakikisha  anamtoa  katika  kifungo  alichojiingiza...

"Unajua  Ray C anampenda  sana  kutokana  na  namna  anavyopenda  kujiweka  kama  yeye na  hata  jinsi  anavyoimba  nyimbo  zake, hivyo  aliposikia  madai  hayo  alianza  kumsaka  kila  kona  lakini  bado  hajafanikiwa  kwani  Rachel  anamkimbia," kimesema  chanzo  hicho.

Hata  hivyo  habari  zaidi  zinasema  kuwa  kutokana  na  namna  Rachel  anavyomuamini  msanii  huyo  wa  kiume  hajakubali  kama  anachanganyiwa  dawa  za  kulevya  kwenye  bangi  na  sigara.

"Mwenyewe  anajiona  yupo  sawa, lakini  sisi  tunaona  tofauti, hakika  Rachel  anapotea  na  sijui  nani  atamuokoa.

"Tumeshamwabia  kwamba  anapotea  lakini  haamini, tunaweza  kusema  kwamba  Ray C aliponea  bahati, sasa  sijui  kama  na  yeye  atapata  bahati  kama  alivyopata  mwenzake, " kilisema  chanzo  hicho

Rachel  ambaye  anatamba  na  wimbo  wa  'upepo'  hakuweza  kupatikana  kuzungumzia  tuhuma  hizo

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger