Hali katika kampini ya RJ inayoongozwa
kwa ubiya kati ya Vicent Kigosi ( Ray) na Blandina Chagula ‘Johari’,
inazidi kuwa tete kwa kile kinachoelezwa kuwa johari hataki kufanya kazi
pamoja na ‘mke mwenza’ Chuchu Hans.
Chanzo hicho ambacho kipo karibu na
wasanii hao kilisema kuwa mwezi mmoja uliopita Johari na Chuchu,
walikuwa katika kuelekea kuelewana ambapo johari, alishakubali yaishe
kuwa Ray wake ameshapokonywa na mtoto huyo wa Kitanga .
Mnyetishaji huyo aliendelea kusema kuwa
baada ya Johari kuwa katika hali hiyo,ndipo Chuchu alipoanza kutanua
makucha yake ndani ya kampuni kwa kujifanya ni mmoja kati ya wakurugenzi
wakati ukweli haupo hivyo.
Chanzo hicho kilizidi kusema kuwa
imefikia hatua Chuchu, kaanza kutoa amri kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo
bila ya kupata kibali kutoka kwa wakurugenzi waasisi ambao mtaji wao
unadaiwa kutokana na Johari ‘kumpiga’ changa la macho mfanyabiashara
maarufu kutoka mkoani Mbeya.
Mpashaji huyo alizidi kusema kuwa bifu
liliibuka upya mkoani Dodoma, ambako Ray na Johari walikwenda katika
ziara ya Kilimanjaro Music Awards Tour, na mashabiki wao kuwataka
wapande jukwaani kwa pamoja.
Mtoa habari hiyo alisema kuwa kuwa
kutokana na hali hiyo, ndipo Chuchu alipoanzisha bifu la chinichini
lililopelekea hadi sasa kwenye kampuni hiyo kuzuka mtafaruku mkubwa huku
Johari, akitaka kujitenga kabisa na Ray lakini kinachomkwamisha ni pesa
zake nyingi alizowekeza.
Inadaiwa kuwa Johari amekuwa mkali sana
sasa hivi akimtaka mkurugenzi mwenzake Ray, wagawane kila kitu mpaka
nguo za ndani walizonunua kwa pesa za kampuni yao hiyo.
Katika kufuatilia habari hizo ili kupata
ukweli kuhusiana na timbwili hili mwanahabari wetu aliwasaka wote
kwenye simu zao za mkononi, lakini wote hawakutaka kutoa ushirikiano kwa
kile walichokieleza kuwa wapo bize na maswala binafsi.
No comments:
Post a Comment