ROSE NDAUKA: TUMEMALIZA BIFU NA JACK CHUZ, SASA KAZI TU!


STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka  amefunguka kuwa kwa sasa yeye na msanii mwenzake, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’  ambaye aliwahi kukwaruzana naye wameshamaliza na kujikita katika kazi zaidi.
Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
Akichonga na paparazi wetu, Rose alisema wamerudi kwa staili ya tofauti kwani kila mmoja anafanya kazi zake lakini wanashirikishana na wana ‘project’ maalum ambayo wataifanya hivi karibuni.
“Mimi na Jack kwa sasa tunafanya kazi hata Wema ambaye tulikuwa naye kwenye kundi moja tukiwa na filamu ya kumshirikisha tutamuita kwa sababu hatuna kinyongo kwani bifu hazijengi kikubwa tunafanya kazi tu,” alisema Rose.
Staa wa filamu Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ kulia akiwa na Rose Ndauka.
Rose na Jack Chuz walipishana kipindi cha nyuma na chanzo kikidaiwa kuwa ni kuibiana mabwana lakini hivi karibuni walimaliza tofauti ambapo walionekana pamoja kwenye msiba wa aliyekuwa muongozaji wa filamu nchini, George Otieno ‘Tyson’.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger