Rubani
wa shirika la ndege ya Afrika Kusini, South African Airways amekamatwa
na askari wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Harare baada ya kuvua nguo
zake zote mbele ya abiria na wahudumu wengine wa ndege hiyo na kubaki na
nguo ya ndani.
Rubani
huyo, W Van Ginkel ambaye alikuwa airushe ndege yenye namba SA 025
kutoka Harare Zimbabwe kuelekea Johannesburg Afrika Kusini, alifikia
uamuzi wa kuvua nguo zake wakati akipita katika eneo la kukaguliwa
abiria, ambapo Baada ya kukaguliwa, akiwa anataka kuondoka kifaa cha
ukaguzi kikatoa mlio, ambapo aliamriwa kuvua viatu.
Hata
baada ya kuvua viatu, kifaa hicho kiliendelea kutoa mlio kila akipita
eneo la ukaguzi, ambapo aliamriwa kutoa mkanda wa suruali yake na
alipofanya hivyo kifaa hicho kiliendelea kutoa mlio hali iliyomkera
rubani huyo na kuamua kuvua nguzo zake zote na kubaki na nguo ya ndani,
hali iliyowalazimu polisi kumkamata.
Kufauatia
tukio hilo, zaidi ya abiria 90 waliokuwa wasafiri na ndege hiyo
walilazimika kusubiri kwa saa tano hadi pale alipopelekwa rubani
mwingine
No comments:
Post a Comment