NI jambo lililowaacha midomo wazi madaktari na wauguzi wa Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam ambapo mtoto Almasi
mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi (pichani akiwa na muuguzi)
kufikishwa hospitalini hapo akiwa amekatwa nyeti na mtu aliyedaiwa ni
mganga wa kienyeji ‘sangoma’ na kuipeleka kusikojulikana.
Akizungumza na Uwazi kwa masikitiko makubwa mwishoni mwa wiki
iliyopita, baba wa mtoto huyo, Ismail Kamaga alisema tukio hilo
lilitokea hivi karibuni katika Kijiji cha Omukagando, Wilaya ya Karagwe
mkoani Kagera.
Alisema sangoma huyo aliyemtaja kwa jina moja la Adinali alifanya
kitendo hicho kwa watoto wawili akidai anawafanyia tohara.“Alidai
anawafanyia tohara watoto wawili, baada ya muda mwenzake alipona wa
kwangu hakuna kitu na nyeti aliondoka nayo, sina namna tena ya
kumsaidia mwanagu.
Nilimpeleka Hospitali ya Mugawa, Kagera ambako aliwekewa mpira wa
kutolea haja ndogo na madaktari wakasema hawana jinsi.“Pia nilikwenda
Kituo cha Polisi Karagwe kuomba msaada wa kumkamata mtuhumiwa lakini
imeshindikana,” alisema baba huyo.
Mzazi huyo aliiomba serikali kumtafuta mtuhumiwa akisema tukio
alilolifanya ni sawa na kuuondoa uhai wa mtu.Kwa upande wake, muuguzi
wa zamu aliyekuwa hospitalini hapo, Kulwa Kaombwe alisema kitendo
kilichofanywa na mtu huyo si cha kuvumiliwa akaiomba serikali kuchukuwa
hatua ili mtuhumiwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
“Kwa ujumla huyu mtoto amebadilishiwa staili ya maisha na hicho ni
kilema. Kumkata uume maana yake mtoto huyo hatapata mke wala watoto
katika maisha yake,” alisema muuguzi huyo.
Kuhusu matibabu, alisema wanaendelea naye lakini tabu anayoipata Almasi ni kujisaidia kwa shida hasa haja kubwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment