Nyota wa filamu Bongo, Yusuph Mlela.
NYOTA wa filamu Bongo, Yusuph Mlela hataweza kuonana
na mpenzi wake ambaye pia ni mzazi mwenzake kutokana na mfungo wa mwezi
mtukufu wa Ramadhan.
Akipiga stori na gazeti hili, Mlela alisema alikuwa na desturi ya kwenda kwa mzazi mwenzake kila siku kwa ajili ya kwenda kumuona mwanaye, Mwantumu lakini kwa mwezi huu itakuwa ngumu kutokana na misingi ya dini yake.
“Futari napikiwa na mama yangu mzazi kwa sababu mwenzangu bado sijafunga naye ndoa, mwanangu akitaka kuniona analetwa nyumbani na mtu anakaa wiki anarudi kwa mama yake,” alisema Mlela ambaye kwa sasa wanafanya kazi pamoja na Hemed Suleiman inayoitwa Enjoy ambayo ni kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
No comments:
Post a Comment