Gari ya Polili ilioibuka kumuokoa Diamond kufuatia sakata la mashabiki wake kupandwa na jazba
Stuttgart,Ujerumani,
Usiku wa Jumamosi ya Tarehe 30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri
Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijikuta katika
hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,ujerumani,baada
ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show,washabiki hao
waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio waliahidiwa kuwa show
ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijikuta wakisubiri hadi majira ya
saa10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na
promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.
Hapo
ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha
chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota
wake,Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu
vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki
kuvunja hadi vyombo vya muziki ma-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini
kwa sasa.
Mmoja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ Flor alipatwa shock mshtuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospatal.
Polisi
nchini ujerumani wanamesema tukio hili la aibu halijawahi kutokea,kuwa
msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari kwani
washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
mpaka
sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa
wanachunguza thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia
itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia
anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.
Magazeti ya Stuttgart; yameandika "Washabiki wa hasira nawe DIAMOND" link:
No comments:
Post a Comment