WIKIENDI iliyopita haikuwa njema kwa mtangazaji
Ephraim Kibonde baada ya kutupwa nyuma ya nondo katika Kituo cha Polisi
cha Oysterbay jijini Dar kwa msala wa kudaiwa kugonga gari na kutoa
lugha ya matusi, Ijumaa Wikienda lina full stori.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini cha habari ambacho kimeshuhudia
sakata hilo mwanzo mwisho, ishu nzima ilianzia maeneo ya Makumbusho
ambapo gari alilokuwa akilitumia Kibonde, liligonga kwa nyuma gari
jingine na kisha kukimbia.
“Baada ya kugonga, Kibonde alirudi nyuma kisha kuanza kukimbia ambapo
trafiki alitumia gari lililogongwa na Kibonde kumkimbiza,” kilimwaga
data chanzo hicho.Chanzo hicho kilifafanua kuwa baada ya polisi
kumkimbiza kwa saa kadhaa, walifanikiwa kumkamata maeneo ya Mwenge
ambapo trafiki alipanda kwenye gari la Kibonde na kumuamuru arudi eneo
la tukio lakini Kibonde hakuwa tayari kurudi ndipo alipoanza kukimbia
tena, huku askari aliyemkamata akiwa ndani ya gari.
“Inaonekana kulitokea kutoelewana kati ya askari na Kibonde ndipo
askari huyo alipowasiliana na wenzie kwa njia ya radio call ili
wambananishe na alipofika Ubungo kwenye mataa wakamtaiti na kumpeleka
kituoni, Oysterbay,” kilihitimisha chanzo chetu.
Baada ya kupata maelezo hayo, kachero wa Ijumaa Wikienda alitia timu
katika kituo cha Oysterbay ili kutaka kujua mustakabali mzima wa ishu
hiyo ambapo alimshuhudia Kibonde akiwa amesimama nyuma ya nondo huku
akiwa anaimba ‘nyimbo’ anazozijua mwenyewe.
Mtangazaji huyo amefunguliwa kesi iliyopewa RB namba OB/RB/13806/20014 KUGONGA NA LUGHA YA MATUSI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment