Kuna
sababu za msingi kabisa kuelezea mambo ya kuzingatia ili kutambua vitu
vitakavyokufanya ufurahie utamu wa ndoa yako. Kuishi na mke au mume sii
kitu rahisi kama ambavyo watu wengi ambao hawako katika ndoa hufikiria.
Hivi ni vipengere baadhi tu, wanandoa na wampenzi wanapaswa
kuvitambua;
Kwanza
kabisa ni kwambie kwamba utamu wa mapenzi sii lazima ufanye tendo la
ndoa ama ngono, kuna mambo kibao ambayo moyo wa binadamu ukiyakosa
huweza kukonda kama muathirika wa magonjwa hatari ya mwili. #"Upendo
kutoka kwa yule umpendae", hili ndilo jambo kubwa la kwanza katika afya
ya moyo ulio katika dimbwi la mapenzi.
Hakuna kitu kitamu kama kupendwa na ukapenda pia, kitendo hiki hufunga
macho yote ya vishawishi vya dunia hii ya kidigitali. Usilazimishe
upendo kwa mtu ambae unaonekana kuwa wewe tu ndiye unaye mjali wakati
yeye hana habari na wewe.
Ndio
maana ukitaka kuingia katika ndoa lazima umtafute mtu unayempenda na
anayekupenda ili muishi katika maisha yasiyo ya kushawishika kufuata
matamanio mengine nje ya ndoa. Kitu cha pili katika kufurahia utamu wa
penzi ni #"amani" watu wengi wana wanaume na wanawake warembo, lakini
hawafurahii mapenzi kwasababu hawana amani ndani ya nyumba.
Utafurahia
utamu wa mahusiano ya ndoa endapo utakuwa na moyo uliopondeka mbele za
Mwenyezi Mungu, yani kuvumiliana katika changamoto za maisha. Wapo watu
wao ni maarufu kwa kuharibu mahusiano ya watu "tofauti na ndugu yako wa
karibu" hakuna mtu anayefurahia kukuona unamwanamke mrembo ndani ya
nyumba au mwanaume mtanashati ndani ya nyumba, na kwambia hili, jifunze
kutunza siri za uzuri wa mkeo au mmeo. Kunawatu wanavitaka vitu hivi
sana hata kwa gharama yoyote ile na popote vitakapopatikana vitanakuwa
halali yao. Kama mpenzi wako anakupa penzi tamu na la kistaarabu, basi
haina haja ya kumueleza rafiki yako maana hujui yeye anakosa nini katika
mahusiano yake na mwenzi wake. Pesa ni silaha kubwa sana
katika
mapenzi haya ya kizazi cha digitali, pesa zimekuwa na ushawishi mkubwa
sana katika mapenzi hivyo unapaswa kuwa msiri katika mambo yako ya
chumbani.
Cha
msingi zaidi, hakuna mtu anayefurahi kusalitiwa katika mapenzi, kila
mtu anatamani kummiriki mwenzi wake asipate wazo la kutoka nje ya
mahusiano. Tunajua kabisa dunia hii kila siku tunakutana na wasichana
warembo kabisa na pia tunakutana na wanaume watanashati sii kidogo,
lakini kitu cha msingi ni kuyashinda macho na kuamini #"UKIONA VYAELEA
UJUE............?
Tukutane katika makala inayofuata.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment