Taarifa toka vyanzo vya kuaminika
zinadai kuwa Menina hivi sasa ndo binti pekee aliyeiteka akili
ya Diamond kuliko wote waliowahi kuwa naye kimahusiano huku
mama mzazi wa Diamond Bi, Snura Kassim akionekana kumkubali kwa
asilimia zote binti huyo….
Vyanzo hivyo vimebainisha kuwa mahusiano ya Menina na Diamond
yamekuwepo kwa miezi kadhaa sasa na Diamond amekuwa na wivu
wa kupindukia juu ya demu huyo kuliko inavyosemekana kwani
amekuwa akimfuatilia kwa kila hatua….
“Hakuna kitu anachokifanya
Menina kwa sasa Diamond asijue, anampenda vibaya utadhani
karogwa na kuna kipindi Diamond alitaka kumzuia asijihusishe na
chochote kwenye Dance 100% kwa kuhofia kuporwa lakini baadae
alikubali aendelee na Dansi 100% baada ya kuhakikishiwa na
dada yake Queen Darling ambaye ni mmoja wa majaji katika
shindano hilo kwamba atamlinda asiguswe na mtu,” kimesema chanzo hicho.
Habari zaidi zinasema kwamba hata
hivi majuzi( kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani) Wema
alipigwa marufuku kushiriki maandalizi ya futari nyumbani kwa
kina Diamond kwa kigezo kuwa taratibu za dini ya kiislamu
haziruhusu hawara kumpikia mwanaume futari lakini Menina alikuwa
akifanya jambo hilo kwa kujinafasi….
“Karibu mwezi mzima
Menina alikuwa akienda kwa kina Diamond na kupika futari, mbali
ya hilo alikuwa akifanya kila alichokitaka katika nyumba hiyo
pamoja na kufanya usafi katika chumba cha Diamond,” kimesema chanzo chetu.
Hata hivyo chanzo chetu kimesema kuwa kuna wakati Diamond aliwahi kusikika akisema kuwa hawezi kumuoa Wema kutokana na rekodi yake ya kuwahi kuwa na mahusiano na watu wengi wanaojulikana nchini hivyo kuwa naye kwa ajili ya kujitangaza kimuziki( kumpatia kiki) tu na muda wa kuoa utakapofika, ataoa binti asiye na umaarufu jijini…..
Kibaya zaidi ni kwamba mama
Diamond ameelezwa kuwa na mapenzi ya dhati na Menina jambo
ambalo linamfanya akose raha pindi Wema anapofika nyumbani
kwake…
Diamond alipotafutwa kupitia simu
yake ya mkononi ili kuzungumzia jambo hilo, simu yake iliita
bila kupokelewa. Wema hakupatikana katika simu zake zote.
No comments:
Post a Comment